Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Vyuo vya Afrika, Norway vyafichua tija tafiti za nishati safi

Дата публикации: 20-10-2026 12:37:16

Watafiti na wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya Afrika na Norway wameeleza mafanikio ya miaka 20 ya ushirikiano katika tafiti za nishati safi na jadidifu, ikiwamo teknolojia za kupikia kwa jua na kuzalisha umeme.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumanne, Oktoba 20, 2026

Profesa Tormdan Nielsen kutoka Norwey akizungumza katika mkutano wa kusherehekea na kufanya tathmini ya miaka 20 ya ushirikiano wa utafiti katika nishati jadidifu Afrika uliofanyika Unguja. Picha na Jesse Mikofu

By  Jesse Mikofu

Mwandishi wa Habari

Mwananchi

Muktasari:
  • Ushirikiano wa miaka 20 umewezesha tafiti, teknolojia za kupikia kwa jua, miradi 17 ya uzamivu na mifumo ya kuzalisha umeme kwa kutumia pampu za maji zilizotelekezwa.

Unguja. Watafiti na wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya Afrika na Norway wameeleza mafanikio ya miaka 20 ya ushirikiano katika tafiti za nishati safi na jadidifu, ikiwamo teknolojia za kupikia kwa jua na kuzalisha umeme.

Mkutano huo wa kutathmini mafanikio ya Mtandao wa Teknolojia ya Nishati wa NORHED II umehusisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Makerere cha Uganda, Eduardo Mondlane cha Msumbiji, Addis Ababa cha Ethiopia, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Norway (NTNU/Trondheim), pamoja na vyuo na taasisi washirika kutoka Malawi na Sudan Kusini.

Akizungumza Oktoba 20, 2026, mtafiti wa NTNU, Profesa Ole Nydal, amesema mradi umejikita katika teknolojia ndogondogo za nishati mbadala, hasa kutumia joto la jua kwa kupikia, kuoka na kuhifadhi vyakula kwa ubaridi.

Amesema mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) umewezesha kuzalisha miradi 17 ya shahada ya uzamivu (PhD), kuandaa mitaala ya pamoja na kuanzisha vituo maalumu vya mafunzo katika vyuo shiriki.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Biashara Malawi, Profesa Ishmael Kosamu akizungunza katika mkutano wa kusherehekea na kutathmini ushirikiano wa utafiti wa nishati safi Afrika. Picha na Jesse Mikofu

Mratibu wa mradi kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya UDSM, Dk Joseph Kihedu, amesema tafiti hizo zinalenga kukidhi mahitaji ya wananchi kupitia nishati ya jua, maji na biomasi.

Amesema watafiti wamebuni mitambo ya kupikia kwa jua inayohifadhi joto kwa matumizi ya baadaye na mifumo ya majokofu ya kuhifadhia chakula. Teknolojia hizo huzingatia vyakula vya jamii husika, vikiwamo maharage, ugali, wali na nyama, huku Ethiopia ikiwa na mfumo maalumu wa kupika injera.

Ameongeza kuwa teknolojia hizo zimeanza kujaribiwa katika mazingira halisi, yakiwamo migahawa ya vyuo vikuu, magereza na kambi za wakimbizi, kwa lengo la kupunguza matumizi ya kuni na ukataji wa misitu, sambamba na kuunga mkono sera za Serikali kuhusu nishati safi ya kupikia.

Mhadhiri wa UDSM na mnufaika wa mradi, Dk Adela Syikilili, amesema ushirikiano huo umewezesha kupata ufadhili wa kuboresha maabara na kupanua mtandao wa kitaaluma wa kimataifa.

Naye Ombeni Mdee, aliyepata shahada za uzamili na uzamivu kupitia mradi huo, amesema utafiti wake wa PhD katika nishati ya maji umewezesha kubuni mtambo unaobadilisha pampu za maji zilizotelekezwa kuwa jenereta na turbine za kuzalisha umeme.

Amesema matokeo hayo yakipewa kipaumbele na Serikali yanaweza kunufaisha jamii, viwanda na matumizi ya nyumbani.

Washiriki wameahidi kuendeleza ushirikiano kupitia mikutano ya kila wiki mtandaoni na kutafuta ufadhili mpya kutoka NORAD na Umoja wa Ulaya ili kuendeleza tafiti na suluhisho za kisayansi kwa jamii za Afrika.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Universidades africanas se alían para potenciar investigación agroforestal y mitigación climática07.830-06-2026
2JSS AHER signs MoU with Japan’s Hokkaido University09.1117-10-2026
3СКФУ и университет Катара договорились о сотрудничестве в области технологий0004-05-2023
4Лесотехнический университет Петербурга договорился о сотрудничестве с вузами Африки0003-08-2023
5«Нанософт» и «Спрут-Технология» объявили о начале совместной работы для бесшовной интеграции проектирования и производства06.3516-10-2026
6«Нанософт» и «Спрут-Технология» объявили о начале совместной работы для бесшовной интеграции проектирования и производства06.3516-10-2026
7Лавров: Россия обсуждает сотрудничество в мирном атоме со странами Африки0020-12-2025
8Университет МИСИС расширяет партнёрство с Намибией0520-03-2026
9Росконгресс и Инновационный центр "Интеза Санпаоло" подписали соглашение о сотрудничестве0026-06-2020

Классификация: Наука. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 6.49. Источник: www.mwananchi.co.tz.