Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar imezindua Sera ya Miji na Makazi inayolenga kudhibiti ukuaji holela wa miji, kuboresha matumizi ya ardhi na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kupata makazi bora, salama na yenye gharama nafuu.
Jumatano, Oktoba 21, 2026

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar, Rahma Kassim Ali akizindua sera ya Miji na Maendeleo ya Makazi Zanzibar, katika ukumbi wa Polisi Ziwani. Picha na Zuleikha Fatawi
Unguja. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar imezindua Sera ya Miji na Makazi inayolenga kudhibiti ukuaji holela wa miji, kuboresha matumizi ya ardhi na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kupata makazi bora, salama na yenye gharama nafuu.
Akizindua sera hiyo leo Jumatano, Oktoba 21, 2026, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar, Rahma Kassim Ali amesema sera hiyo itaweka dira, mwelekeo na mfumo wa pamoja wa kusimamia ukuaji wa miji, upangaji wa matumizi ya ardhi na maendeleo ya makazi nchini.
Amesema sera hiyo inalenga kukabiliana na changamoto za ujenzi usiozingatia mipango miji, matumizi yasiyofaa ya ardhi na migogoro inayotokana na hali hiyo, ambayo pia huathiri upatikanaji wa huduma za kijamii na miundombinu.
“Tumezoea kuona ukuaji wa miji usiozingatia mipango ya matumizi ya ardhi, ujenzi holela na matumizi yasiyofaa ya ardhi, hali ambayo imeendelea kusababisha kuongezeka kwa migogoro ya ardhi katika jamii. Sera hii itakuwa mwarobaini wa changamoto hizo,” amesema.
Kuhusu upatikanaji wa makazi, Waziri huyo amesema nyumba bora na zenye gharama nafuu bado ni hitaji muhimu linalohitaji mikakati endelevu ya kisera pamoja na ushirikiano wa wadau mbalimbali.
Amesema ni muhimu kuweka mifumo itakayowawezesha wananchi wa makundi tofauti kupata makazi yanayokidhi mahitaji yao, huku sera hiyo ikisisitiza ushiriki wa Serikali na sekta binafsi katika kubuni mifumo ya uwekezaji na ufadhili wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
Ameongeza kuwa mafanikio ya sera hiyo yatategemea utekelezaji wake, akieleza kuwa imeweka mipango inayobainisha mahitaji ya rasilimali zitakazohitajika kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, amewataka wananchi na masheha kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa sera hiyo kwa kufuata na kuzingatia mipango ya matumizi ya ardhi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Khadija Khamis Rajab, amesema mchakato wa kuandaa sera hiyo ulianza mwaka 2023, ukifuatia tathmini iliyofanyika mwaka 2020 kupitia ripoti ya Diagnostic Report for the Zanzibar Urban Policy, iliyoainisha changamoto mbalimbali na kubainisha umuhimu wa kuwa na sera maalumu ya kusimamia upangaji na maendeleo ya miji.
Amesema changamoto zilizoibuliwa katika tathmini hiyo ni pamoja na ujenzi usiozingatia mipango miji, kusambaa kwa makazi ya msongamano mdogo katika maeneo mapana, uhamaji wa watu, uhaba wa nyumba zinazomudu gharama za wananchi, msongamano katika baadhi ya maeneo ya makazi, ongezeko la idadi ya watu, upungufu wa miundombinu na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ameeleza kuwa sera hiyo inashughulikia maeneo mbalimbali, yakiwemo utawala wa ardhi, upangaji na uendelezaji wa miji na makazi, sekta ya miliki, utunzaji wa mazingira, miundombinu, huduma za kijamii, usimamizi na udhibiti wa ujenzi, ongezeko la idadi ya watu na uhamiaji.
Maeneo mengine ni maandalizi na kukabiliana na maafa, ulinzi na usalama wa pamoja pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi zinazohusika na usimamizi wa miji na makazi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi, Laila Burhan Ngozi, amesema migogoro ya ardhi ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili kwa kiasi kikubwa katika maeneo yao.
Amesema uzinduzi wa sera hiyo ni hatua muhimu inayotarajiwa kusaidia kukabiliana na migogoro hiyo na kuimarisha usimamizi wa matumizi ya ardhi.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Rais Mwinyi atangaza ufadhili wanafunzi watakaopata daraja la kwanza Zanzibar | 0 | 10 | 21-10-2026 |
| 2 | Bima ya Afya kwa Wote II kulenga kaya 625,000 | 0 | 5.98 | 22-10-2026 |
| 3 | Safari ya nishati safi inavyokumbana na mikingamo | 0 | 5.95 | 24-08-2026 |
| 4 | Для восстановления жилья и соцобъектов в Иркутской области создана отдельная структура | 0 | 0 | 24-07-2019 |
| 5 | Минстрой внес в правительство программу развития индивидуального жилищного строительства | 0 | 0 | 22-07-2019 |
| 6 | Минстрой продолжит работу по сокращению строительного цикла | 0 | 0 | 14-05-2025 |
| 7 | Минстрой стимулирует запуски проектов по строительству жилья в новых регионах | 0 | 0 | 19-03-2025 |
| 8 | ГКУ «СевВодРесурсы» займется защитой города от паводков | 0 | 7.74 | 10-08-2026 |
| 9 | ДОМ.РФ и институты развития займутся формированием городской среды Сахалина и Геленджика | 0 | 0 | 07-06-2019 |