Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

TotalEnergies yaimarisha usalama wa wanafunzi Buguruni Viziwi

Дата публикации: 03-09-2026 15:21:05

Wanafunzi 264 wa Shule ya Msingi Buguruni Viziwi wameanza kunufaika na jiko la kisasa linalotumia nishati safi ya kupikia pamoja na alama za usalama barabarani, baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa kitaifa wa Mpango wa Usalama Barabarani wa VIA mwaka 2025.

Основное содержимое страницы с новостью.

Dar es Salaam. Wanafunzi 264 wa Shule ya Msingi Buguruni Viziwi wameanza kunufaika na jiko la kisasa linalotumia nishati safi ya kupikia pamoja na alama za usalama barabarani, baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa kitaifa wa Mpango wa Usalama Barabarani wa VIA mwaka 2025.

Huduma hizo zimekabidhiwa na TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa lengo la kuboresha usalama wa shule na mazingira yake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo leo Alhamisi, Septemba 3, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile, amesema mpango huo unaonyesha mchango wa wanafunzi katika kuimarisha usalama wa jamii.

‎Muonekano wa jiko la zamani linalotumia Kuni lililopo katika Shule ya Buguruni viziwi. Picha na Jumanne Bakana.

Mpangile amesema tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2022 kwa ushirikiano na TotalEnergies Foundation na Nafasi Art Space, umewafikia zaidi ya wanafunzi 32,000 katika shule 60 za Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Pwani.

Amesema jiko hilo linaunga mkono Mkakati wa Serikali wa Nishati Safi ya Kupikia unaolenga kufikisha matumizi ya nishati hiyo kwa asilimia 80 ifikapo 2034.

Mkuu wa Dawati la Elimu Barabarani kutoka Makao Makuu ya Polisi, Mbunja Matibu, amepongeza uwekezaji huo kwa watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa wito kwa sekta binafsi kuiga mfano huo.

‎Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Buguruni viziwi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa jiko la gesi ikiwa ni sehemu ya tuzo ya shule hiyo, kuibuka mshindi wa kitaifa wa Mpango wa Usalama Barabarani wa VIA kwa mwaka 2025. Picha na Jumanne Bakana.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Richard Kweka, amesema awali wanafunzi walikuwa katika hatari ya ajali kutokana na ukosefu wa alama za kutosha, akieleza kuwa mwaka jana mwanafunzi mmoja aligongwa na pikipiki na kupoteza meno mawili.

Kweka ameomba mamlaka za barabara kuweka tuta eneo hilo ili kusaidia kupunguza mwendo wa magari.

Kuhusu jiko hilo, amesema limeongeza ufanisi katika mafunzo ya vitendo ya upishi, huku maji ya lita 60 sasa yakichemka kwa dakika 45, tofauti na ilivyokuwa kwa matumizi ya kuni.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Shule ya Kalangalala kutumia nishati safi06.8727-08-2026
2Likizo ya El Nino fursa wazazi kuwashupalia watoto madrasa09.1122-10-2026
3Всероссийская акция "Урок безопасности" пройдет в школах со 2 по 8 сентября0027-08-2019
4В Тверской области реализовано больше 50 проектов Программы поддержки школьных инициатив в 2026 году010.1203-08-2026
5East Africa: Tanzania Unveils Plans to Supply Natural Gas to Uganda, Kenya Through Pipelines06.1927-07-2026
6В Ингушетии создадут новые "Кванториумы" и "IT-кубы" для школьников0005-11-2020
7Всероссийский урок безопасного интернета для школьников пройдет 24 января0020-01-2022
8Ставропольских школьников научат безопасно передвигаться на самокатах и сигвеях0029-08-2019
91 сентября 2026 начинаем с Разговоров о важном и Урока ...011.101-09-2026
10🚨 Учебная тревога: проверка на прочность пройдена! 🚨 В нашей ...06.516-09-2026

Классификация: Пресс-релизы. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 7.65. Источник: www.mwananchi.co.tz.