Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Staa wako Bongo naye ana staa wake mamtoni

Дата публикации: 26-09-2026 13:31:40

KUPTIA mahojiano mbalimbali, baadhi ya mastaa wa Bongofleva wamewahi kuwataja wasanii kutoka nje ambao wanawashabikia au waliowavutia hadi na wao kuamua kufanya muziki.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumamosi, Septemba 26, 2026

By  Peter Akaro

Mwandishi

Mwananchi Communication Limited

Muktasari:
  • Wanamuziki kama Celine Dion, Michael Jackson na Beyonce, wamekuwa chachu au mfano wa kuigwa kwa wanaotaka kufanya muziki, na pia wamekuwa na mashabiki wengi wa kazi zao. Fahamu zaidi.

KUPITIA mahojiano mbalimbali, baadhi ya mastaa wa Bongofleva wamewahi kuwataja wasanii kutoka nje ambao wanawashabikia au waliowavutia hadi na wao kuamua kufanya muziki.

Wanamuziki kama Celine Dion, Michael Jackson na Beyonce, wamekuwa chachu au mfano wa kuigwa kwa wanaotaka kufanya muziki, na pia wamekuwa na mashabiki wengi wa kazi zao. Fahamu zaidi.

1. Diamond Platnumz: Kipindi akiwa na ndoto ya kufanya muziki, msanii wa nje aliyemvutia na kumtazama kama mfano wa kuigwa kwake ni Usher Raymond IV, mshindi wa Grammy mara nane aliyepata umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 kupitia albamu yake ya pili, My Way (1997). 

2. Vanessa Mdee: Waimbaji wa kike mashuhuri duniani kama Alicia Keys, Whitney Houston, Lauryn Hill, Toni Braxton, Celine Dion, Monica, Destiny's Child, Aaliyah, Mary J. Blige na Mariah Carey, ndio waliomvutia Vanessa kufanya muziki ingawa sasa ameacha muziki.

3. K-Lynn: Ni mshindi wa Miss Tanzania 2000, anasema tangu akiwa mdogo alikuwa akiwatazama Mariah Carey na Whitney Houston wakiimba live, naye akatamani siku moja aje afikie viwango hivyo. Na kweli akaja kufanya vizuri katika Bongofleva kupitia nyimbo zake kama Nalia kwa Furaha, Crazy Over You, Nikipata Wangu, Nipe Mkono, Mr. Blue na Chochote Utapata.

4. Banana Zorro: Kabla ya kuibuka mshindi wa Tanzania Pop Idol 2001, tayari Banana Zorro alikuwa akijifunza mengi kutoka kwa Michael Jackson ambaye hadi sasa ameuza rekodi zaidi ya milioni 400 duniani, huku akishinda tuzo 15 za Grammy kipindi cha uhai wake.

5. AY: Mwanachama huyo wa East Coast Team, anajitambulisha kama shabiki mkubwa wa kazi za mtayarishaji muziki, Dr Dre, aliwahi kueleza moja ya ndoto zake ni kuja kukutana naye na hata kufanya kazi pamoja. Dr Dre ni Mkurugenzi Mtendaji wa Aftermath Entertainment ambayo imefanya kazi na wasanii wakali kama Eminem, Kendrick Lamar, Busta Rhymes, Snoop Dogg, The Game, 50 Cent na kadhalika.

6. Lady Jaydee: Baada ya kizazi cha kina Whitney Houston kupita, Jide anamtaja Rihanna kama mwanamuziki wa kike aliyekuja miaka ya hivi karibuni ambaye amemvutia. Anasema melodi za Rihnna kwake amezipa maksi za asilimia 100.

7. Sugu: Mkongwe huyu wa rap Bongo, ni shabiki mkubwa wa Jay Z kiasi kwamba aliamua kumpa mtoto wake wa kwanza wa kiume jina la Shawn, ambalo ndilo la kuzaliwa la Jay Z akiitwa Shawn Corey Carter.

8. Lulu Diva: Licha ya kutangulia kuigiza, ila bado ndoto yake kubwa ilikuwa ni muziki, huku wasanii wa nje waliowahi kumpa hamasa wakiwa ni Celine Dion na Beyonce Knowles ambaye ni mke wa Jay Z.

9. Shaa: Kabla ya kuweka rekodi kama msanii wa kwanza wa kike kusainiwa MJ Records, Shaa alivutiwa na Aaliyah, Brandy, Toni Braxtin, Mary J. Blige, Whitney Houston na Madonna. Hiyo ni baada kumsikia dada yake akisikiliza nyimbo za wasanii hao kila mara.

10. Dudu Baya - Alianza muziki mwaka 1999, wakali waliomvutia ni 2Pac na DMX ambao walivuma sana miaka 1990, na kwa sasa wawili hao tayari wote wamefariki. 2Pac aliteka masikio ya wengi zaidi duniani kupitia albamu yake ya nne, All Eyez on Me (1996), huku DMX akifunika kupitia albamu yake ya pili, X (1999) iliyojumuisha wimbo wake maarufu, Party Up (Up in Here).

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1FEROOZ: Miaka 21 ya 'Starehe' na bado unaishi010.3924-09-2026
2Basata yamshushia rungu Dudu Baya, mratibu wa Bongo Flava 30010.3426-09-2026
3Singeli 'kichaka' kinachompa maisha D Voice06.4826-09-2026
4Rany Kida; King of Dance mwenye simulizi moto ya dansi09.0724-09-2026
5Ran Kida: Kutoka Kagera hadi kutawala majukwaa ya dance Tanzania01023-09-2026
6Rweyemamu agusia kiwango cha Chilambo01019-09-2026
7Neema Kusekwa: Mgore, Manula wampa maujanja07.6626-09-2026
8Baleba njia yake Man United yahitaji subira08.0625-09-2026
9Kwa nini Kuminga kaichagua Wolves badala ya Lakers?06.3226-09-2026
10UEFA yaonya soka Ulaya, yagawanyika08.4425-09-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 9.37. Источник: www.mwanaspoti.co.tz.